Ze Comedy wabwagwa kortini

August 20, 2008

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha biashara, jana ilitupilia mbali ombi la kundi la sanaa za vichekesho la Ze Comedy kutaka mahakama hiyo itoe idhini ya wao kuendelea na kazi zao kwa kutumia jina hilo wakati kesi ya msingi ikiendelea.

Katika ombi hilo la awali, wasanii hao wakiongozwa na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga’, waliiomba mahakama hiyo kutoa zuio kwa kituo cha televisheni cha East Africa, EATV na Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA), kutowazuia wao kufanya kazi kwa jina la Ze Comedy.

Akitoa uamuzi huo jana, Jaji wa mahakama hiyo, Catherine Urio, alisema ili mahakama iweze kutoa zuio, lazima kitu kinachogombewa kiwe katika hali fulani.

Jaji huyo alisema, katika hoja zote zilizoletwa mahakamani hapo na walalamikaji (wasanii) na EATV (walalamikiwa), hakuna yeyote aliyeonyesha kutumia alama ya Ze Comedy kwa sasa, ingawa wadaiwa wa kwanza, EATV, wameomba kuwa wamiliki wa jina hilo kwa mdaiwa wa pili (COSOTA), lakini bado ombi hilo halijatekelezwa.

Aliongeza kuwa, walalamikaji (Ze Comedy), walikuwa na kibali cha kulitumia jina hilo la Ze Comedy Production kwa mwaka mmoja, kuanzia Julai mosi mwaka 2007 hadi Juni 30 mwaka huu.

Alisema, licha ya kibali cha wasanii hao cha kutumia jina la Ze Comedy kwisha, hakuna maombi ya kibali kingine, huku EATV wakiwasilisha maombi COSOTA kutaka kupewa umikili wa jina la Ze Comedy.

Jaji alisema, kwa mazingira, mahakama inatakiwa kutoa uamuzi kwa uangalifu mkubwa pasipo kuingilia hoja za kesi ya msingi ambayo bado haijaanza kusikilizwa.

Alisema kutokana na hilo, mahakama imeona si sahihi kisheria kwa sasa kuruhusu kazi na jina la Ze Comedy kuendelea kutumika kabla ya kesi ya msingi haijaamuliwa.

Kuhusu madai ya wasanii wa Ze Comedy kutaka EATV iwalipe fidia ya usumbufu katika uamuzi wa ombi la awali, mahakama pia imetupa ombi hilo.

Baada ya kutupwa kwa ombi hilo la awali, kesi ya msingi sasa itaanza kusikilizwa Oktoba 21.

Wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Ze Comedy, baada ya kujiondoa katika umiliki wa EATV na kuhamia TBC1, EATV wakawazuia wasanii hao kutumia jina hilo na majina yao na vionjo walivyokuwa wakitumia awali.


Blogsphere: TechnoratiFeedsterBloglines
Bookmark: Del.icio.usSpurlFurlSimpyBlinkDigg
RSS feed for comments on this post
 |  TrackBack URI for this post

Comments

5 Responses to “Ze Comedy wabwagwa kortini”

  1. james mcharo on September 11th, 2008 12:53 pm

    ze comedy msijali kama vp badilisheni 2 jina kwani 2meshawajua hata mkibadilisha jina soko lenu halitapungua litabaki palepale kama ndio nia yao kuwaaribia wameula machuya

  2. furaha maugo on September 11th, 2008 12:56 pm

    ze comedy group kazeni boot mtashinda tu kama namna gani vp badilisheni jina anzeni kazi m2pe burudani wa2 wenu,au co

  3. Nasor alkindy on September 13th, 2008 6:05 pm

    Badilisheni jina haina kwele soko litasimama tu au vip mazee!

  4. Arafat Karama on December 28th, 2008 9:31 pm

    Heey ze comedi mnalipa wenyewe binafsi na sio jina kama vp badilisheni jina na sisi kama watazamaji tutawasapoti vilevile kama kawa. sie tunawamaindi nyinyi na sio jina vipaji mnavyo kwani japo tupo mbali na home still tunawakubali na kuwa fagilia kama desturi ama vipi kudadadeki kandamizeni kibara mwendo wa robot mtatoboa.

  5. Amina on March 19th, 2009 9:50 pm

    Jamani ze comedy tumewamiss hata huku ughaibun tunawafagilia mbona serikali inatuumiza. Kiss baby don’t loose your work¨!

Got something to say?