Shirikisho la kandanda wakili Tanzania haikuwa tayari kwenda Ghana

January 29, 2008

WAKATI michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiendela nchini Ghana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela, amesema ilikuwa ni ndoto kwa Tanzania kucheza fainali hizo kutokana na kutokuwa na mkakati wa muda mrefu katika soka la vijana.

Mwakalebela aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam na kusema kwa nchi ambayo haikuwa na mkakati wa kukuza vijana kama Tanzania ni ndoto kubwa kushiriki fainali hizo na zile za dunia zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2010.

“Ninachoweza kusema TFF tumejifunza jinsi ya kuandaa mashindano kama haya katika nchi yetu kwa ukanda mzima wa CECAFA” alisema Mwakalebela

“Katika nchi 15 za Afrika zenye viwanja vizuri Tanzania ni miongoni mwao, mchakato mzima wa ndoto yetu kwenda Ghana imetuamsha usingizini na kututoa matongotongo.

“Ingekuwa ni ndoto kwenda huko na si Tanzania tu nchi zote ambazo hazina mkakati wa kukuza vijana tumeona jinsi zilivyoshindwa kufuzu fainali hizo.

Katika nchi za ukanda wa CECAFA Sudan pekee ndiyo iliyofuzu kucheza fainali hizo lakini hata hivyo imefungashiwa virago na Misri baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Mafarao hao wa Misri.

“Kama TFF tumejua nini cha kufanya tumetoka gizani sasa hivi tuna programu ya vijana na tunajikita katika hili kuhakikisha tunafuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2010.


Blogsphere: TechnoratiFeedsterBloglines
Bookmark: Del.icio.usSpurlFurlSimpyBlinkDigg
RSS feed for comments on this post
 |  TrackBack URI for this post

Comments

Got something to say?