Sasa nataka Mkanda – ‘Tyson’

December 21, 2007

BONDIA chipukizi wa Tanzania katika ngumi za kulipwa uzani mwepesi ‘Fly’, Shabani Madilu ‘Tyson’, kesho anatarajia kupanda ulingoni kuonyeshana kazi na Selemani Bwamkuu katika pambano lisilo la ubingwa la raundi nane, litakalofanyika katika Ukumbi wa Maridadi Pub Kinondoni, Dar es Salaam. Akizungumza jana kwenye Ukumbi wa New Vijana ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam anakojifua bondia huyo alisema kwa sasa hapendi kuendelea kucheza mapambano yasiyo ya ubingwa na anachohitaji kwa sasa ni heshima ya kuwa bingwa.

Tyson aliyasema hayo wakati akielezea maandalizi yake ya mpambano wake wa kesho baada ya Jumamosi iliyopita kumtwanga kwa KO raundi ya 4, bondia Shabani Rajab wa Dar es Salaam, katika pambano lisilo la ubingwa lililopigwa katika Ukumbi wa Luxury Pub Temeke, Dar es Salaam.

Alisema kiwango cha pesa wanachokipata kwa kazi hiyo ya masumbwi ni kidogo sana ambacho hakilingani na kazi yenyewe, hivyo kitu pekee kinachoweza kuwafariji mabondia ni heshima ya kutwaa mkanda.

“Nimechoka kupigana mapambano yasiyo ya ubingwa, nawaomba mapromota waniandalie mapambano ya ubingwa,” alisema Tyson

KUTOKA: TANZANIA DAIMA


Blogsphere: TechnoratiFeedsterBloglines
Bookmark: Del.icio.usSpurlFurlSimpyBlinkDigg
RSS feed for comments on this post
 |  TrackBack URI for this post

Comments

Got something to say?