Nigeria, Benin hoi Ghana

January 27, 2008

HUKU nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba akiiongoza timu yake kuifunga Benin 4-1 juzi, Nigeria ilishindwa kufungana na Mali katika mechi za kundi B. Kwa ushindi huo, Ivory Coast sasa imefikisha pointi sita, hivyo kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali.

Mali iliyotoka sare na Nigeria katika mechi ya pili iliyopigwa hiyo juzi, imefikisha pointi nne na itahitaji pointi moja kuingia robo fainali itakapokwaana na Ivory Coast mechi ya mwisho.

Nayo Nigeria yenye pointi moja itamaliza na Benin ambako ili kusonga mbele inatakiwa kuishinda kwa wastani mzuri wa mabao huku ikiomba Mali ipoteze kwa Ivory Coast.

Katika mechi ya kwanza hiyo juzi, Drogba ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia bao timu yake katika dakika ya 40.

Dakika moja kabla ya mapumziko, Ivory Coast ilipata bao la pili likifungwa na Yaya Toure huku bao la tatu likifungwa na Abdul Keita.

Aliyepigilia msumari wa mwisho katika lango la Benin, ni Aruna Dindane katika dakika ya 63.

Benin ilipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 90, likifungwa kwa kichwa na Razak Omatoyossi.

Mechi za fainali hizo, zitaendelea leo kwa timu za kundi D, kushuka dimbani ambako Senegal itakwaana na Angola huku Tunisia ikicheza na Afrika Kusini.


Blogsphere: TechnoratiFeedsterBloglines
Bookmark: Del.icio.usSpurlFurlSimpyBlinkDigg
RSS feed for comments on this post
 |  TrackBack URI for this post

Comments

Got something to say?