Maximo: Ni ngumu Timu ya Taifa Brazil kuja Tanzania

January 26, 2008

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa Taifa Stars , Marcio Maximo amesema suala la kuja kwa timu ya taifa ya Brazil kuweka kambi hapa nchini wakati ikienda Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia bado ni gumu.

Hayo yalisemwa jana na kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Marcio Maximo alipozungumza na waandishi wa habari jana na kusema ana imani Shirikisho la soka Tanzania, TFF na Brazil, FBC zitawasiliana kuhakikisha timu hiyo inakuja Tanzania.

Maximo aliyekwenda mapumzikoni nchini Brazil alisema alipokuwa nyumbani, alitumia siku kadhaa kuzungumza na viongozi wa chama cha soka cha nchi hiyo kuhusiana na ujio huo na Chama hicho kilimpa orodha ya vitu wanavyotaka kutimiziwa ili waweze kuja hapa ingawa kuna vitu vingi na vigumu

Kocha huyo alisema anatarajia kuwaita wachezaji wazoefu kuunda Taifa Stars akiwemo mshambuliaji wa Simba, Athumani Machuppa na kusema atapata nafasi tu endapo ataonyesha uwezo kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union.

“Lakini pamoja na uwezo wake anatakiwa kuwa na nidhamu kwani ndiyo inambeba mchezaji yeyote anapokuwa uwanjani, aingie aonyeshe uwezo wake uwanjani na nidhamu.

“Awali wakati kila mtu anazungumzia kuhusu Machuppa ndio alikuwa amefika tu na hajacheza mchezo hata mmoja nisingeweza kumwita kwa kuwa nilikuwa sijamuona nah ii siyo timu ya mtaa bali ya taifa,” alisema.

Juu ya Athuman Idd, Maximo alisema kuwa mchezaji huyu kipindi kile alikuwa na matatizo ya kinidhamu lakini endapo ataonyesha uwezo wake ule ule kwenye mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Ashanti anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wake.

Wakati huo huo, Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na Malawi Februari 6 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa mguu ( TFF) Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa wamekuwa wakiwasiliana na nchi nyingi za Afrika lakini hadi jana Malawi ndio pekee iliyothibitisha.

Alisema kuwa mechi hiyo ipo katika program ya FIFA ya michezo ya kirafiki na wanaendelea kushughulikia gharama mbalimbali za timu hiyo ambayo wachezaji wake wawili, Wisdom Ndlovu na James Chilapondwa wanaichezea Yanga ya Dar es Salaam watakuwemo.

Alisema TFF italazimika kugharamia kila kitu kwa timu hiyo ikiwa ni pamoja tiketi za ndege , malazi na chakula na usafiri wa ndani.

Kocha wa Stars, Marcio Maximo yuko katika harakati za kusuka na kuimarika kikosi chake kwa ajili ya kampeni za kufuzu kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA limewateua waamuzi wanne wa Tanzania kuchezesha mchezo kuwania kufuzu kwa fainali za Olimpiki itakazofanyika nchini China kati ya Afrika Kusini na Nigeria utakaofanyika mjini Pretoria Februari 16.

Mwakalebera alisema waamuzi hao ni Isabellah Kapera ambaye ni mwamuzi wa kati, wasaidizi ni Zahara Mohamed Sumwa na Saada Hussein Tibabimale wakati Judith Gamba atakuwa mwamuzi wa akiba.

Aliongeza kuwa nalo Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika CAF limeteuwa Tanzania kuteuwa waamuzi watakaochezesha mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika na kati ya URA ( Uganda) na Zesco United ( Zambia) utakaofanyika Februari 16 nchini Uganda.

Alisema kuwa kutokana na uwamuzi huo kamati ya waamuzi TFF imewatauwa Oden Mbaga, Hamis Chang’walu na Juma Ally Kombo na Pascal Chiganga, john Longinal Kanyenye na Haji Makame watachezesha mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Rwanda.


Blogsphere: TechnoratiFeedsterBloglines
Bookmark: Del.icio.usSpurlFurlSimpyBlinkDigg
RSS feed for comments on this post
 |  TrackBack URI for this post

Comments

Got something to say?