Binti Kiziwi - Z-Anto
October 19, 2007
Katika anga za Tip Top Connection ni kona ambayo imesheheni vijana wenye sauti nzuri na walio na vipaji katika muziki kundi hili maskani yake ni jijini Dar es salaam mnatusoma? Kama ilivyo kawaida vijana hawa Studio yao ni Bongo Record ikiwa chini ya producer P Funk.
Kuna kijana mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Z Anto..Umeshasikia Mpenzi jini? jamaa anakamua ile kichizi japo kuwa mambo yake anayoyafanya si sawa na umri wake kwani kiumri bado ni mdogo sana lakini mambo yake ni bab kubwa.
Ally Mohamed ndio jina halisi la kijana huyu..Mnatusoma……jamaa alizaliwa miaka 19 iliyopita na kwa upande wa elimu ndio kwanza anasema bado yupo katika hali changa kwani anatarajia kwenda masomoni mwakani mungu akipenda.
Anasema ” Elimu yangu niliipata katika shule ya msingi Tungi iliyopo huko Kigamboni Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es salaam….Jamaa anasema kuwa nilizaliwa na kukulia katika Wilaya hiyo mpaka hivi sasa ambapo tayari nimeshaingia katika masuala ya muziki.
Je wajua… Kijana anasema kuwa sasa tayari ameshayaona mafanikio yaliyopo katika kazi na ni tofauti angekuwa tu mtaani na washkaji kwani anajifunza mengi ikiwemo na utafutaji katika maisha. Z Anto ana haya ya kusema je ni yapi hasa….. Hebu msome.
”Niliingia katika sanaa kutokana na kupenda sana muziki na hasa hasa niliupenda licha ya mwanamuziki wa Marekani R Kelly kunivutia zaidi mpaka nikaamua nami nijaribu kwani kuimba ni dhamira tu. Baada ya hapo ndipo nilipoanza kutunga mashairi yangu mwenyewe na kujikuta nikiweza kutengeneza verse zilizokuwa bora na nzuri tu, ambazo nahisi mashabiki wangu wanazipenda pia tena sana tu.
”Nyimbo yangu ya kwanza ambayo niliimba na ilikuwa ndio mwanzo wangu ipo kwenye Albamu yangu ambayo nilishaipeleka sokoni toka Julai mwaka huu na mpaka sasa bado inafanya vizuri. Waweza ndio nyimbo yangu ya kwanza na baada ya hapo ndipo nilipogundua kuwa kumbe kuimba naweza na pia wengi walinipa sapoti”.
Dah baada ya Starehe kutaka kujua ni mawazo gani hasa yalimpelekea kuweza kuimba wimbo wa Mpenzi Jini Z Anto anasema ” Unajua sister nini hii bwana ni sanaa unajua kuwa nilipata tu Idea (mawazo) kichwani wakati nilipokuwa nikipanga mashairi yangu.
”Unajua bwana hii kitu ni kwamba ilikuwa ya kawaida tu kwani idea yangu niliwaza hasa nifanyeje ili nitoke tofauti ila dah…. Idea hii ilikuwa ni ngumu sana kwangu kutokana na uhalisia wake lakini nilikuwa nayo mda mrefu sana lakini baadae niliamua kuimba wimbo huo” alisema.
Kutokana na jamaa huyu kuwa na kivutio hasa katika sauti yake na apokuwa akiimba ukifuatilia zaidi utagundua kuwa jamaa anakuwa katika uhalisia fulani….Jamani taratibu si ya kweli hayo ni sanaa tu mwanawane… unajua bwana kuna watu wengine wanajenga uhalisia kuwa kijana huyu yamemtokea la hasha!.
Habari kubwa kuhusiana na jamaa ni kwamba akiwashirikisha washkaji zake kadhaa katika kuhakikisha kuwa anatoka vizuri anasema ” kwa hivi sasa nipo katika maandalizi ya kuanza kuandaa video yangu ya kwanza kabisa ambayo itakuwa ni Binti Kiziwi hii itafungua ukurasa kwangu na ni nyimbo ambayo ipo katika albamu yangu ambayo nimeshaiachia sokoni tayari” unamsikia ?…anaongeza kuwa
Nafanya video ya Binti kiziwi baada ya kuisha mwezi mtukufu wa ramadhani nitakuwa tayari nimeshaiachia. Nimeamua kufanya hivyo kwa kusudi tu kwani nadhani mawazo ya wengi yatakuwa ni kwa nini nisifanye ya Mpenzi jini ila ni uamuzi wangu mimi nikishirikiana na Boss wangu anasema.
Unajua nini jamaa hivi sasa ameamua kufanya kitu hicho kwanza, kwani anasema kuwa hivi karibuni na ni baada ya kuachia video ya Binti kiziwi ataanza filamu ya Mpenzi jini ambayo bado hawajapanga na hakuwa tayari kusema kuwa ni wasanii gani ambao watashiriki na itaanza lini matengenezo.
Dah!! ila jamaa anapata tabu sana msome kwanza….??Tangu nisimame katika fani hii nimekuwa nakosa sana uhuru japo kuwa watu wengi hawanifahamu lakini wapo wachache ambao wananifahamu. Inaweza ikawa ni safari ya nusu saa lakini nikatembea zaidi ya hapo kutokana na usumbufu njiani lakini kwangu inanitia nguvu na kuniongezea imani kuwa kumbe nakubalika katika sanaa hii inanifariji kwa kweli??.
Katika kuona kuwa elimu yake bado ni ndogo Z anaamua sasa kwenda shule kwani katika kukaa kwake anasema anakosa raha sana anapoona kuwa hana elimu ya kutosha…” mwakani nimedhamiria kwenda shule kwa kuwa elimu yangu ni ndogo sana, lakini siwezi kuacha muziki nitaendelea nao kama kawaida.
Ni kijana mdogo sana lakini kutokana na mafanikio aliyoyapata kupitia muziki yameweza kubadilisha mfumo wa maisha yake, ikiwa ni pamoja na kuwa na gari ya kutembelea.
Licha ya hiyo mshkaji ana haya ya kusema kuhusiana na wizi wa kazi za wasanii anasema?Wizi upo na kwa kweli sidhani kama utaisha kwa kuwa hata kama una hatui miliki, kwani kila mtu ana malengo yake katika maisha.
Anasema kuwa inategemea na ugumu wa maisha katika hali halisi ya sasa hivi kwani kuna baadhi ya watu wengine sanaa ya muziki sasa wanaichukulia kama ni sehemu ya kujipatia maslahi, kuwaibia nyimbo wasanii, kuvujisha nyimbo zao kwa kweli hili si haki.
Blogsphere: TechnoratiFeedsterBloglines
Bookmark: Del.icio.usSpurlFurlSimpyBlinkDigg
RSS feed for comments on this post | TrackBack URI for this post
Comments
20 Responses to “Binti Kiziwi - Z-Anto”
Got something to say?


Ninapenda wimbo wake sana na swali yangu ni je, ninaweza kupata maandishi yani lyrics za binti kiziwi wapi?
Ahsante sana.
I’M A KENYAN LADY AND I THINK OF ALL THE SWAHILI SONGS I HAVE LISTENED TO, HAKUNA NYINGINE ISHAWAHI KUNIZUZUA KAMA BINTI KIZIWI.
THE SINGER HAS NOT ONLY THE MESSAGE BUT ALSO HIS VOICE LEAVES ME WANTING TO LISTEN TO HIM MORE AND MORE.
THIS GUY IS TALENTED WHY LIE!
manze uko poa sana zidi kushtua watu
The dude sings out of His heart.Keep it up.u look nice.
the guy is just talented
yaani ninastaajabu kila mara ninapousikia wimbo huo! Nami pia nataka maandishi ya “Binti Kiziwi”. someone just send the link!!
Ebwanaa wimbo wa Mpenzi jini unatesa sana, ila kinacho nishangaza ni kwanini uliamua kuimba kuhusu majini???
mimimkwa kweli nimshabiki wa binti kiziwz nataka kujuwa anafanya kazi gani?
I rily lyk da song and its 2 attractive. Very talented guy. Unapendeza kweli!!
I SPEECH SWAHILI,KIRUNDI AND FRENCH I COME FROM CANADA.NAPENDA KUULIZA HUYO BINTI(SISILI) NIKWELI NIKIXIWI?
KWAMAANA MIMI NAPENDA KUSOMA HABALI ZA KWETU HUKO AFRICA
i am isak from nairobi-kenya really i am flirted wit this song though i could prefer to get the lyrics please send me the lyrics of Binti Kiziwi mr A-zanto..
thanks
am akenyan but binti kiziwi ana kipawa ya kuimba na kutunga wimbo. Hongera sana.
This dude resembles my ex LIKE WOW!!!! everytime i miss him, all i have to do is watch the video 1001 times n am set tho i end up wishing i hadn’t!! that’s real talent right there……………….. kip it up n blazing dude!! u got what it takes!!!!
well the guy z good yani we need the lyrics,otherwise this guy z off the hook
Twarusha hands up and voice up kwako Z -anto kwa maana hivyo ndivyo sauti yapashwa kua.Na tena mashairi yaliomo katika mziki wako Binti kiziwi,yame tulia.Kwahio BIG UP nyingi Z-anto.
does anyone knoe where i can download i love it sooooooooooooooooo much!!!
plz ppl do you know?
oh must be mp3 fomat
this guy is talented go on zanto,usisahau kunitumia maadishi the
song is very touching.
Ee bwana! This is what we call talent! Loo, na jamaa wa Red & Yellow t-shirt…. don’t mention. its a great great song. the words are well chosen & the beats are soul soothing…
Basi wenzangu kule Kenya mwasema ni? Hapo mpepigwa 10 nil… plse try bonga route..
Bongo juu, Bongo juu sana!!!
AM STUDENT AT MKU IN THIKA,KENYA.Z ANTO YOU VERY MUCH CREATIVE TO COMEUP WITH SUCH SONG, AND YOUR VOICE,TOGETHER WITH THAT OF PINGU MAKES ME LISTEN BINTI KIZIWI OVER AND OVER AGAIN.