KILA LA KHERI NASREEM
December 13, 2008

Leo ni fainali za kumtafuta mrembo wa dunia wa mwaka 2008(Miss World 2008). Shindano hilo linafanyikia nchini Afrika Kusini ndani ya jiji maarufu la Johanesburg katika ukumbi ujulikanao kama Sandton Convention Centre.Tanzania inawakilishwa na mrembo wetu Nasreem Karim(pichani).
Shindano la mwaka huu ambalo mwanzoni lilikuwa limepangwa kufanyikia huko Kiev nchini Ukraine kabla ya kuhamishiwa Afrika Kusini kutokana na mgogoro wa kisiasa uliokuwa unafukuta baina ya majirani Georgia na Urusi,limevunja rekodi ya kuwa na washiriki wengi kushinda miaka mingine yote katika historia ya miaka 58 ya shindano hilo.Jumla ya washiriki 109 wanashiriki shindano la mwaka huu.
Mrembo wa dunia wa mwaka jana,Zhang Zilin kutoka China ndiye anatarajiwa kumkabidhi mrembo mpya wa dunia taji.BC inamtakia kila la kheri Nasreem Karim ambaye katika mashindano hayo anajulikana zaidi kwa jina la Nasreem Ndiye.Kila la kheri.
from BONGO CELEBRITY @ BONGO CELEBRITY
Related Articles
Comments
Got something to say?










